May 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaipiga Mwadui, yaipumlia Yanga kileleni

Spread the love

 

GOLI pekee lililofungwa dakika ya 66 na Nahodha John Bocco wa Simba ya Dar es Salaam dhidi ya Mwadui FC, limewafanya kufikisha pointi 52 na kusogea kileleni mwa ligi hiyo ya mwaka 2020/21. Anaripoti Matrida Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Ushindi huo, unawafanya mabingwa hao watetezi Simba, kuwasogelea vinara wa ligi hiyo, Yanga yenye pointi 54 ikiwa imecheza mechi 25 huku Simba yenyewe ikiwa imecheza michezo 22.

Ikiwa Simba itacheza viporo vyake vitatu vilivyobaki na kujikusanyia pointi tisa, itafikisha pointi 61 na kuwaacha watani zao Yanga kwa pointi saba.

Simba imeibuka na ushindi huo mwembamba dhidi ya Mwadui FC, leo Jumapili tarehe 18 Aprili 2021, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Kambarage, mkoani Shinyanga.

Mechi inayofuata itacheza na Kagera Sugar uwanja wa Kaitaba kisha Gwambina ya mkoani Mwanza.

error: Content is protected !!