May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaipiga Kaizer Chiefs 3, yaaga mashindano

Spread the love

PAMOJA na ushindi wa bao 3-0 walioupata kkabu ya Simba dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, lakini mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wameaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 4-3. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Simba ambao walipoteza mchezo wa kwanza wa robo fainali uliochezwa Afrika Kusini wiki iliyopita kwa mabao 4-0, walikuwa wanahitaji ushindi wa mabao 5-0.

Kampeni ya Simba kusaka tiketi ya nusu fainali katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ilianza dakika ya 23 kwa John Bocco kuandika bao la kwanza na kufanya mchezo kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Simba walirudi kwa kasi kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 56 akiunganisha krosi fupi ya Mohammed Hussein.

Wakati Kaizer Chiefs wakicheza mchezo wa kuzhia zaidi huku wakipoteza muda, Simba waliendelea kulisakama lango la wapinzani wao na kufanikiwa kupata bao la tatu kupitia kwa Claytous Chama dakika ya 85.

Hadi kipenga cha mwisho matokeo yalibaki kuwa Simba mabao matatu ambayo yameshindwa kuwasaidia kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

error: Content is protected !!