January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaipiga 3-0 Red Arrows, Morrison usipime

Spread the love

 

TIMU ya Simba ya Tanzania imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Red Arrows ya Zambia katikap Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo, umepigwa leo Jumapili, tarehe 28 Novemba 2021, kuwania kuingia hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika huku ikishuhudia Red Arrows mchezaji wake akipigwa kandi nyekundi.

Ni mchezo ambao umeshuhudia Bernard Morrison akicheza kadanda safi na lenye kuvutia kwa kufunga magoli mawili, kutoa pasi ya goli pamoja na kukosa mkwaju wa penati.

Dakika 90 zimemalizika kati ya 180 ambapo, tarehe 5 Desemba 2021, Simba watasafri kwenda Zambia kwee mchezo wa marejeo na kuhitmisha dakika zingine 90.

Mchezo huo wa leo, umeshuhudia ukichezwa huku mvua ikinyesha kipindi chote cha kwanza na kupunguza radha ya mpira kwani wachezaji walikuwa wakiteleza ama mpira kutuama kwenye maji.

Dakika 16, Bernard Morrison aliiandika Simba bao la utangulizi kwa mira wa adhabu nje ya 18, baada ya yeye mwenyewe kuchezawa vibaya na walinzi wa Red Arrows.

Simba ikiendelea kuliandama lango la Arrows, dakika tatu baadaye, Morrrison aliwachambua vilivyo mabeki na kumpasia Meddie Kagere na kuukwamisha kimiani.

Licha ya uwanja kutokuwa rafiki kutokana na mvua kunyesha hivyo maji kuwapo kwa baadhi ya wanna, Simba ilikuwa ikicheza kwa kunana na dakika 30, Morrison aliyekuwa kwenye kiwango bora, alıkosa mkwaju wa penati kwa kupanguliwa na kipa wa Red Arrows.

Penati hiyo, ilitokana na Hassn Dilunga kuangushwa ndani ya 18 na Simba, ikaenda mapumziko ikiwa mbele kwa magoli 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kushambuliana kwa zamu na dakika 57 ilishuhudia kadi nyekundi kwa mlinzi wa kushoto wa Red Arrows, Prosper Chiluya baada ya kumchezea fail, Israel Mwenda.

Simba ikiwa na uchu wa magoli, iliendelea kushambulia na dakika 77, Morrison aliwaacha walinzi wa Arrows na kupiga shuti na kumpiga ‘tobo’ kipa wa Arrows na kuiandikia goli la tatu.

Hadi dakika 90 zinamalizika, Simba 3-0 na mchezo wa marejeo utapigwa tarehe 5 Desemba 2021 nchini Zambia.

error: Content is protected !!