August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaingia mkataba mnono, yavuta milioni 300

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba imeingia mkataba na kampuni ya Emirates Aluminium leo 21 septemba 2021 katika makao makuu ya Emirates Aluminium Sinza, Dar es salaam kwa ajili ya kutoa motisha kwa wachezaji watakao fanya vizuri ndani ya mwezi na mwaka kwa ujumla katika klabu hiyo.anaripoti Damas Ndelema na Wiston Josia Tudarco(endelea)…

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya makubaliano hayo,Mmtendaji  mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez amesema kuwa wameingia rasmi mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Emirates Aluminium ili kutoa motisha kwa wachezaji watakao fanya vizuri ndani ya mwezi na mwaka kwa ujumla pia mkataba huo unathamani ya shillingi milioni 300 utaendelea kudumisha mahusiano mazuri baina ya Simba na Emirate Aluminium

‘’ leo tumeingia mkataba wa miaka miwili na Emirates Aluminium ili kutoa motisha kwa wachezaji na mkataba huu una jumla ya thamani ya sh. milioni 300.’’ alisema Barbara

Mkataba huo wa miaka miwili utatoa motisha kwa wachezaji watakao fanya vizuri katika klabu hiyo, kutakua na tuzo za mchezaji bora kila mwezi na kutakuwa na mchezaji bora wa mwaka kwa ujumla , kipa bora , na mfungaji bora pia jambo hili halitakua geni kwani tayari taasisi hizi zilikua zilishaanza utaratibu huo toka msimu uliopita kwa kutoa tuzo za mchezaji bora wa mwezi na kwenda msimu ujao wameboresha kwa kutoa mchezaji wa mwezi, mwaka, kipa bora na mfungaji bora

Aidha tuzo hizo za mwezi zinapatikana kwa mashabiki kwa kupiga na kuchagua mchezaji wanaeona amefanya vizuri kwa mwezi husika na mchezaji atakae pata kura nyingi ndo atashinda.

error: Content is protected !!