May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaimngia mkataba na Emirates

Spread the love

 

KLABU ya Simba imeingia mkataba na kampuni ya Emirates Aluminium Profile ambao watakuwa wanatoa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, ambaue atakuwa anapigiwa kura na mashabiki kuanzia Machi 2021. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkataba huo umesainiwa hii leo tarehe 17 Machi, 2021 jijini Dar es Salaam huku upande wa Simba ukiwakilishwa na Afisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara kwa niaba ya mtendaji mkuu wa timu hiyo Barbara Gonzalez.

Wakati wa tukio hilo Manara alisema kuwa tuzo hizo zimelenga kutoa nafasi kwa mashabiki wachague mchezaji bora wao kwa kila mwezi.

Aidha msemaji huyo aliendelea kusema kuwa kwenye tuzo hizo watazingatia takwimu za kila mchezaji huku wadhamini wao kampuni ya Emirates Aluminium Profile wakitoa kiasi cha Sh. 1 milioni pamoja na tuzo.

“Yatatolewa majina kutokana na takwimu na kura hizo zinataanza kupigwa kuanzia mwezi wa tatu, wenzetu wa Emirates watatoa tuzo pamoja na kiasi cha shilingi milioni moja kila mwezi,” aliongezea msemaji huyo.

Aidha uongozi wa klabu hiyo, ulisema zoezi hilo la kupiga kura litafanyika kupitia akaunti za klabu hiyo kwenye mitandao ya kijamii na kura hizo zinapigwa ndani ya siku tatu na mshindi wa tuzo atatangazwa kila tarehe tano ya mwezi husika.

Tuzo hizo zitakuwa tofauti na zile zinazotolewa na wadhamini wa Ligi Kuu, Kampuni ya simu ya Vodacom ambao wanatoa tuzo hizo kila mwezi kwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

error: Content is protected !!