July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaifumua Ruvu 3-0, Azam yaipumulia Yanga

Wachezaji Simba wakishangilia moja ya mabao waliyofungwa katika mchezo wa leo

Spread the love

TIMU ya Simba imerudisha matumaini ya mbio za ubingwa baada ya kuitandika Ruvu Shooting mabao 3-0, huku Azam FC ikiendelea kuipumulia Yanga kwa kuitandika Coastal Union 1-0. Anaripoti Erasto Stanslaus … (endelea).

Simba ambayo ilifungwa na Mgambo mabao 2-0 katika mchezo wao wa mwisho, lakini leo imewafuta machozi mashabiki wake katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Azam wao walikuwa jukwaani jana wakati Yanga ikizidi kupaa kileleni katika mchezo wao dhidi ya Mgambo waliovuna ushindi wa mabao 2-0, nao leo wamepata pointi tatu wakiikaribia Yanga kwa tofauti ya pointi moja. Yanga imeongoza Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 37.

Simba kwa ushindi huo imefikisha pointi 32 ikiwa katika nafasi ya tatu, shukrani kwa mabao ya Ibrahim Hajib dakika ya 60, Awadh Juma dakika ya 61 na Elias Maguri 76.

Bao la Azam lilifungwa na nahodha wake, John Bocco na kuifanya timu yake kuondoka na pointi tatu muhimu katika mechi yao ya ugenini.

Katika mchezo mwingine uliochezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu za Sokoine, kati ya Prisons na Polisi Morogoro umemalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya kumalizika kwa suluhu.

error: Content is protected !!