May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaifuata Yanga fainali Kombe la Mapinduzi

Spread the love

MABAO ya Meddy Kagare na Miraji Athumani yalitosha kuipeleka Simba kwenye fainali ya kombe la Mapinduzi baada ya kuiondosha Namungo FC kwenye mchezo wa nusu fainali. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Fainali hiyo itachezwa siku ya Jumatano tarehe 13 Januari, 2021 ambapo itawakutanisha vigogo wa soka nchini klabu za Simba na Yanga ambao wote walikuwa.washiriki kwenye michuano hiyo.

Simba ilipata bao kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Meddy Kagere dakika ya 6 na bao la pili likifungwa na Miraji Athumani dakika ya 40, huku bao la kufutia machozi kwa Namungo likifungwa na Steven Sey na kufanya mchezo huo kumalizika kwa jumla ya mabao 2-1.

Kwa matokeo haya Simba inaifuata Yanga kwenye fainali ambayo ilimtoa Azam FC kwa mikwaju ya Penati 5-4, baada ya sare ya bao 1-1, kwenye dakika 90 za kawaida.

Hii itakuwa mara ya pili kwa timu hizo kukutana fainali kwenye kombe la Mapinduzi ambapo mara ya mwisho Simba ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0, mabao yaliyofungwa na Mussa Mgosi

Lakini pia hii itakuwa mara ya pili kwa timu hizo kukutana toka kuanza kwa msimu wa 2020/21, ambapo mchezo pekee waliokutana ulikuwa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na kumalizika kwa kufungana bao 1-1.

error: Content is protected !!