November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yafufua matumaini Klabu Bingwa

Spread the love

BAO la Meddy Kagere katika dakika ya 64 ya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba dhidi ya Al Ahly kutoka Misri lilitosha kufufua matumaini ya kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Simba ambayo ilionekana kupoteza matumaini hapo awali baada ya kupoteza katika michezo miwili ya ugenini dhidi ya AS Vital na Al Ahly ilijitahidi kupambana katika dakika zote 90 za mchezo kwa kumiliki mpira asilimia kubwa na hatimaye wakaibuka na ushindi.

Baada ya mchezo kumaliza kocha wa klabu ya Simba Patrick Aussems alisema alitumia muda mwingi kuwaonesha wachezaji wake video ya mchezo waliopoteza Misri kwa mabao 5-0 na kuona namna gani wanaweza kurekebisha makosa.

“Niliwaonesha baadhi ya video ni kivipi Al Ahly wanacheza na tukaweza kujipanga vizuri na tulikuwa na mipango mizuri na tumebakisha mechi mbili na tutaona matokeo yake,” alisema kocha huyo.

Baada ya ushindi huo sasa Simba inafikisha jumla ya pointi sita baada ya kushinda michezo miwili na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi D.

https://www.youtube.com/watch?v=KJnmjfIktgU&feature=youtu.be

error: Content is protected !!