January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaendeleza uteja kwa Mbeya City

Wachezaji wa Mbeya City wakichuana na Simba

Spread the love

TIMU ya Simba SC leo imedhihirisha kuwa ‘wateja’ kwa Mbeya City baada ya kukubali tena kichapo cha mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu za Sokoine, jijini Mbeya. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Simba imekutana na Mbeya City mara nne, ambapo haijawahi kuwafunga timu hiyo lakini imekubali kupoteza michezo mitatu, na msimu huu imepoteza michezo yote miwili. Mechi ya mzunguko wa kwanza Simba ilifungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa.

Mabao ya Mbeya City leo yamefungwa na mshambuliaji wake hatarj Paul Nonga wakati la pili lilifungwana Peter Malyanzi.

[pullquote]

MATOKEO YA MECHI ZA LEO:

Mbeya City 2-0 Simba
Azam FC 2-1 Kagera Sugar
Stand United 1-1 JKT Ruvu
Polisi Moro 2-0 Ndanda

[/pullquote]

Kwa matokeo hayo Simba imezidi kupoteza matumaini ya mashabiki wake ya kushika nafasi ya pili kwa kuwa sasa tofauti ya pointi kati yake na Azam imekuwa ni pointi saba kwa kuwa Azam leo imefikisha point 42 na Simba imebaki na point zake 35.

Mechi ya Simba inayofuata ni dhidi ya Azam FC itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii.

 

error: Content is protected !!