May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yabanwa mbavu na Mtibwa Sugar

Spread the love

WEKUNDU wa Misimbazi Simba leo tarehe 22, Januari 2022 wameshindwa kutamba mbele ya Mtibwa Sugar baada ya kutoka suluhu 0-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Manungu Turiani Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu .. (endelea)

Katika mchezo huo uliokuwa na matumizi ya nguvu kupita kiasi, umewakosesha mashabiki ladha ya uhondo wa soka kutokana na uwanja huo wa Manungu kujaa maji baada ya mvua kunyesha.

Aidha, mashabiki wa Simba kwa mara nyingine walifarijika baada ya kumuona mchezaji wao kipenzi, ‘Mwamba wa Lusaka’ Clatous Chama akicheza mechi ya kwanza tangu arejee kwenye Simba.

Chama aliingia kwa kipindi cha pili, aliiwezesha Simba kubadilisha mchezo kwa Simba na kuanza kufika mara kwa mara kwenye langu la Mtibwa Sugar lakini bahati mbaya bahati haikuwa kwa wekundu hao.

Simba sasa inafikisha alama 25 baada ya kucheza michezo 12 na mahasimu wao Yanga wanaendelea kubaki kileleni na pointi  32, kesho  itashuka dimbani dhidi ya Polisi Tanzania katika Uwanja wa Sheikh Amr Abeid Arusha.

 

error: Content is protected !!