KIKOSI cha wachezaji 25 wa Simba pamoja na viongozi kimewasilini jijini Khartom nchini Sudan kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Merreikh huku muda wa kuchezwa mchezo huo ukibadilika kutoka saa 3 usiku na sasa utachezwa majira ya saa 10 kwa saa za Afrika mashariki na saa 9 kamili kwa saa za sudani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Mabadiliko ya muda huo yamethibitishwa na mtendaji mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalenz kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika kuwa “Tupo njiani kuelekea Khartoum, Sudan kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merreikh, muda wa mechi umebadilika”
Simba imewasili leo alfajili nchini Sudan na kuanza maandalizi ya mchezo huo wa kundi A, ambapo mpaka sasa wao ndio vinara kwenye kundi hilo wakiwa na pointi sita mara baada ya kuibuka na ushindi katika michezo yao miwili ya awali, dhidi ya As Vita na Al Ahly.
Al Merreikh wanaingia kwenye mchezo huo huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza katika mechi mbili za awali mara baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wa kwanza na baadae kufungwa mabao 4-1 kwenye mchezo wa nyumbani dhidi ya AS Vita kutoka Congo.
Leave a comment