October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaanza kwa sare, Bocco akosa penati

Spread the love

 

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Simba ya Dar es Salaam, imeanza msimu mpya wa ligi kuu 2021/22 kwa droo dhidi ya Biashara United. Anaripoti Mitanga Hunda, TUDARCo…(endelea).

Mchezo huo, umepigwa Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara leo Jumanne, tarehe 28 Septemba 2021.

Katika mchezo huo, umeshuhudia nahodha wa kikosi cha Simba, John Bocco akikosa penati dakika ya 90+3 kwa kipa kuipangua.

Mara baada ya mchezo huo, Kocha msaidizi wa Simba, Suleiman Matola amesema, wanamshukuru Mungu kwa kumaliza mchezo.

“Tunashukuru kwa mchezo, kutokana na uwanjani tumebadili mchezo na kutufanya tubadili mchezo, lakini haikuwa bahati kwetu kwani hadi penati tumepata lakini ndiyo hivyo.

Naye kocha mkuu wa Biashara,Patrick Odhiambo amesema, tunawashukuru wachezaji kwa kucheza vizuri na kutuwezesha kupata alama moja na sasa tunajipanga kwa mechi nyingine.

error: Content is protected !!