August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaahirisha kuzindua jezi

Spread the love

 

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2020/21, Simba ya jijini Dar es Salaam, imetangaza kuahirisha shughuli ya uzinduzi rasmi wa jezi zao watakazotumia msimu ujao wa 2021/22. Anaripoti Hunda Mintanga, TUDARCo…(endelea).

Simba ilipanga kufanya uzinduzi huo kuanzia saa 1 usiku, tarehe 4 Septemba 2021, jijini Dar es Salaam.

Imetangaza kuahirisha shughuli hiyo ikiwa ni simu moja tangu jezi hizo kutambulishwa hadharani na uongozi wa Simba na kampuni inayozizalisha na kuziua ya Vunja Bei.

“Tukio la uzinduzi wa jezi rasmi za Simba kwa msimu wa 2021/22 lililopangwa kufanyika leo limeahirishwa. Matukio yote ya sherehe sasa yatafanyika wakati wa Wiki ya Simba inayoanza 13-19 Septemba 2021,” imeeleza taarifa ya Simba.

Jana Ijumaa, Simba ilizitangaza jezi hizo ambazo tayari zimeanza kuuzwa katika maduka mbalimbali ya Vunja Bei nchi nzima.

Kilele cha Wiki ya Simba ‘Simba Day’ kitafanyika katika Uwanja wa Benjamini Mkapa mkoani Dar es Salaam ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali ikiwemo kutambulisha wachezaji waliosajiliwa kwa msimu ujao.

error: Content is protected !!