Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari Simba ya kimtaifa hatarii, yaibamiza ASEC mabao matatu
HabariMichezo

Simba ya kimtaifa hatarii, yaibamiza ASEC mabao matatu

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba imeanza vizuri kampeni yake kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, kufuatia kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, dhidi ya ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo wa kundi D, ulipigwa hii leo tarehe 13 Februari, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, majira ya saa 10 jioni ambapo ulikuwa mchezo wa kwanza wa Simba kwa msimu huu.

Uwepo wa John Bocco uwanjani ambaye aliingia  kipindi cha pili cha mchezo huo, akichukua nafasi ya Meddie Kagere zilitosha kumfanya kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo, kufuatia kuhusika katika mabao mawili ya ushindi.

Bao la kwanza la Simba katika mchezo huo, lilifungwa kwa ustadi mkubwa na kinda Raia wa Senega Pape Ousman Sakho kwa njia ya Tik taka, mara baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Peter Banda kwenye dakika ya 12.

Kipindi cha pili kiliporejea Simba ilionekana kucheza kuimalika, licha ya ASEC kuonekana kucheza vizuri kiasi cha kupelekea kupata bao la kuchomoa kupitia kwa Aziz Ki Kwenye dakika 60.

Mara baada ya kuchomoa bao hilo, kocha mkuu wa klabu ya Simba Pablo Franco Martini ndipo alipofanya mabadiliko na kumuingiza Uwanjani, nahodha wa kikosi hiko John Bocco ambaye alionekana kuwa lulu mara baada ya kuhusika katika mabao mawili ya mwisho.

Dakika ya 79, Shomari Kapombe alifanikiwa kuiandikia Simba bao la pili kwa njia ya mkwaju wa penati kufuatia Bocco kufanya kazi kubwa.

Baada ya kupachika bao hilo, zilichukua dakika mbili Simba kuandika bao la tatu kupitia kwa Banda mara baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Bocco ambaye alibadilisha mchezo toka alipoingia dimbani.

Mara baada ya kukamilika kwa dakika 90 za mchezo huo kocha mkuu wa klabu ya Simba, Pablo alifunguka kuwa timu yake ilitengeneza nafasi nyingi lakini hazikufanikiwa kutumika vizuri.

“Tulicheza vizuri, lakini tulitengeneza nafasi nyingi kama ya Banda na Kagere lakini zilishindwa kutumika, lakini pamoja na yote niwapongeze wachezaji walicheza vizuri.” Alisema kocha huyo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

error: Content is protected !!