Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari Simba wazindua rasmi wiki yao, majibu ya jezi yapatikana
HabariMichezoTangulizi

Simba wazindua rasmi wiki yao, majibu ya jezi yapatikana

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Simba hii leo tarehe 31 Julai 2022, imezindua rasmi wiki yao kuelekea kwenye tamasha kubwa la Siku ya Simba (Simba Day), ambayo itaambatana na shughuli mbalimbali. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Uzinduzi huo umefanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem, na kuhudhuriwa na viongozi sambamba na wanachama na mashabiki wa klabu hiyo.

Katika uzinduzi uliambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo Zuhura Othuman, maarufu kama Zuchu kutoka Wasafi.

Tamasha hili linakuwa kama mlango kuelekea msimu ujao wa mashindano, na mara nyingi hutumika kama sehemu ya kutambulisha kikosi sambamba na benchi la ufundi mbele ya mashabiki.

Akielezea mipango yao kuelekea msimu ujao Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa, klabu hiyo kwa msimu ujao wa mashindano 2022/23, itakwenda kurejesha makali yake yaliyopotea kwenye msimu uliomalizika huku wakija na kauli mbiu ya kwamba hawazuiliki.

“Nimetoka kule Misri na kitu muhimu ilikuwa kujipanga kwa ajili ya msimu unaokuja, malengo ya klabu yapo palapale tunarudi kwa nguvu tunarudi kurudisha ubingwa wetu, na kauli mbiu yetu kwa msimu huu itakuwa, hatuzuiliki wala hatushikiki,” amesema Barbara.

Kwenye msimu uliomalizika ambao kikosi hicho kilikuwa chini ya kocha Pablo Franco Martin ambaye alifungashiwa virago ndani ya klabu hiyo, hawakufanikiwa kuchukua taji lolote na kuwa na msimu mbaya katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.

Pia uongozi huo uliweka wazi viingilio kwa siku ya tamasha hilo litakalofanyika tarehe 8 Agosti, 2022, ambapo kiingilio cha chini kitakuwa Sh. 5000, huku kiingilio cha juu kikiwa ni Sh. 30,000.

Tamasha hilo litafanyika jijini Dar es Salaam, kwenye dimba la Benjamin Mkapa kuanzia majira ya asubuhi.

Matukio ya wiki hii yataenda sambamba na uzinduzi wa jezi mpya zitakazotumika kwa msimu ujao, ambapo Mwenyekiti wa klabu hiyo Murtaza Mangungu ameweka wazi kuwa jezi za Simba kwa msimu huu zitatoka Ulaya na sio tena nchini nchina.

“Kuhusu jezi msimu huu tumeacha kwenda kule hung haa (China), safari hii tumekwenda Ulaya, jezi zetu za safari hii zitakuwa zimetoka Ulaya na sio tena Asia na wiki hii tutazindua na tutakuwa vizuri,” amesema Mangungu.

Wakati hayo yote yanafanyika bado uongozi wa klabu hiyo haujaweka wazi, watakwenda kucheza na timu gani kwenye siku hiyo kama sehemu ya mchezo wa kirafiki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!