KESHO Mafahari wawili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu za Simba na Yanga, zinashuka dimbani kusaka pointi tatu, huku kila upande ukijinasibu kutoka na ushindi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)
Mchezo huo, utapigwa leo Tarehe 3 Julai, 2021 kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, majira ya saa 11 jioni ambapo Simba atakuwa mwenyeji wa mchezo huo.
Kuelekea mchezo huo, kocha msaidizi wa kikosi cha Simba Seleman Matola, alisema kuwa Kesho, wamakwenda kuchukua pointi tatu, ili kutetea taji hilo kama walivyjiwekea malengo mwanzoni mwa msimu huu.
“Maandalizi yetu yanakwenda vizuri, kama tulivyoahidi mwanzo wa msimu nia yetu nikutetea vikombe vyetu vyote vitatu, na tayari kimoja tunaenda kukitangaza katika mechi inayokuja.” Alisema Matola
Kama Simba ataibuka na ushindi kwenye mchezo huu wa leo dhidi ya watani wao, klabu ya Yanga, watatangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara nne mfululizo.
Simba anaingia kwenye mchezo huo, huku akiwa kileleni kwenye msimamo huo, akiwa na pointi 73, mara baada ya kucheza michezo 29, nafasi ya pili ikishikwa na Yanga waliocheza michezo 31, wakikusanya pointi 67.
Leave a comment