Thursday , 2 February 2023
Home Kitengo Michezo Simba wasaini mkataba na ATCL
Michezo

Simba wasaini mkataba na ATCL

Spread the love

 

UONGOZI wa Klabu ya Simba SC na Shirika la Ndege nchini Tanzania (ATCL) wameingia mkataba wa ushirikiano wa kibiashara ambao utakuwa na manufaa kwa pande zote. Anaripoti Damas Ndelema TUDARCo … (endelea).

Mkataba huo utaiwezesha Simba kusafiri ndani na nje ya Tanzania kwa ndege za shirika hilo pekee ikiwa katika safari zake.

Mkataba huo wa miaka miwili umesainiwa leo tarehe 17 Septemba 2021 mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam

Akizungumzia mkataba huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema mkataba wa ushirikiano una thamani ya Sh. 400 milioni.

Amesema mazungumzo yalianza tangu mwezi Aprili mwaka huu na leo ndio wamefikia tamati ya makubaliano na shirika hilo.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania, Mhandisi Ladslaus Matindi amesema kuwa klabu ya Simba itatumia huduma za safari za Ndege za ATCL ndani na nje ya nchi.

“Simba watakapokuwa na safari za ndani na nje ya nchi watatutangaza na sisi maana Simba ni brand kubwa na ndicho kilicho tuvutia… pia jezi za Simba queens zitakua na nembo yetu pembeni usawa wa mkono hii yote ni ushirikiano baina yetu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!