July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba wang’ara tuzo za mwezi VPL

Spread the love

KOCHA mkuu wa klabu ya Simba Patrick Aussems na mshambuliaji wake, Miraji Athuman wameibuka vinara wa tuzo za mwezi Septemba za Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/20. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Miraji amefanikiwa kushinda tuzo hiyo baada ya kumshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, baada ya kuwashinda mwenzake wa klabu ya Simba Meddy Kagere na Ismail Kada kutoka Tanzania Prisons, wakati Aussems ameshinda tuzo ya kocha bora baada ya kuwabwaga makocha Mohammed Rishard wa Prisons na Abdallah Mohammed Baresi wa JKT Tanzania.

Aussems amefanikiwa kushinda tuzo hiyo baada ya kufanikiwa kuingoza Simba kushinda michezo minne ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kufanikiwa kukusanya jumla ya pointi 12 na kufanya timu hiyo kuwa kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Kwa upande wa Miraji ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwa katika kiwango kizuri kwa kufanikisha timu yake kupata ushindi mbele ya Mtibwa Sugar baada ya kufunga bao la pili sambamba na kutoa pasi mbili za mabao na hivyo atazawadiwa kiasi cha Sh. 1,000,000 kutoka kwa mdhamini wa mkuu wa Ligi.

error: Content is protected !!