October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba wamtema rasmi Aussems, mwenyewe athibitisha

Spread the love

KOCHA wa Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji amethibitisha kuvunjwa kwa mkataba wake na klabu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Baada ya kuwepo kwa tetesi za muda mrefu pamoja na vikao vya mara kwa kati nya uongozi wa klabu hiyo na Aussems, hatimaye leo uongozi umempa barua ya kuvunja mkabata.

Aussems alikiri kupokea barua ya kuvunja mkataba wake kwa kuandia kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa ameitwa na Mkurugenzi wa klabu hiyo na kumpa barua ya kuvunja mkataba wake.

“Mkurugenzi Mkuu na bodi ya Simba, wamenitaarifu kuwa kuanzia sasa mimi sio kocha wa Simba,” aliandika hivyo Aussems.

Miongoni mwa tatizo lililomuondoa kikosi kocha huyo ambaye aliifikisha Simba hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita ni kuondoka nchini bila kufuata taratibu za ruhusa kwa waajiri wake.

Juzi Alhamisi, uongozi wa klabu ya Simba chini ya Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingiza uliitisha kikao ambacho Aussems alihudhuria ili kujieleza lakini maswali yote aliyoulizwa ilidaiwa alishindwa kuyatolea ufafanuzi ikiwemo kwanini aliondoka pasipo kufuata utaratibu, alikwenda wapi na kufanya nini.

error: Content is protected !!