Spread the love

 

HATIMAYE klabu ya Simba imempa mkono wa kwaheri kiungo wake mshambuliaji Bernard Morrison, Raia wa Ghana ambaye atakauwa nje ya kikosi hiko hadi mwishoni mwa msimu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Katika taarifa yao waliyoitoa hii leo tarehe 13 Mei 2022, klabu ya Simba ilieleza kuwa kwa makubaliano ya pnde zote mbili wameamua kumpa mchezaji huyo mapumziko mpaka mwisho wa msimu huu ili ashughulike na mambo yake binafsi.

Aidha sehemu ya taarifa hiyo ilieleza kuwa, klabu ya Simba inamtakia mchezaji huyo mapumziko mema na safari yake ya soka hapo baadae, jambo ambalo limeonesha tayari klabu hiyo imeachana na mchezaji huyo.

Kabla ya kutolewa kwa taarifa hii, Morrison hakuonekana katika michezo miwili ya Ligi Kuu mfululizo bila uongozi wa klabu hiyo kutoa taarifa yoyote.

Mara ya mwisho mchezaji huyo kuonekana uwanjani ilikuwa tarehe 30 Aprili 2022, kwenye mchezo wa watani wa jadi ambapo Simba ilishuka uwanjani kuikabili Yanga, mchezo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.

Hii ni mara ya pili kwa klabu ya Simba kumsimamisha mchezaji huyo, ikumbukwe katika miezi mitatu iliyopita klabu hiyo ilimsimamisha mchezaji huyo kwa utovu wa nidhamu kufuatia kushindwa kuripoti kaambini kwa wakati na kisha baadae kumsamehe.

Morrison ambaye alijiunga na Simba tarhe 8 Agosti 2020, akitokea Yanga mara baada ya kuingia kwenye mgogoro mzito wa kimkabata.

Akiwa ndani ya uzi wa Simba Morrison alitumikia klabu hiyo katika michezo 43 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, huku kwa upande wa Yanga alicheza michezo 16 katika kipindi cha nusu msimu

Kwenye kipindi hiko cha miaka miwili na miezi miwili akiwa kama mchezaji ndani ya klabu za Simba na Yanga, Morrison alikosekana kwenye michezo 43, kwa sababu tofauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *