November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba wamlilia Akilimali Yahya

Spread the love

 

KLABU ya Simba imepata pigo baada ya kuondokewa na mchezaji wake wa zamani Akilimali Yahya kilichotokea usiku nwa kumkia leo katika Hospitali nya Rufaa Maweni mkoani Kigoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba leo tarehe 30 Oktoba, 2021 jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa mchezaji huyo amefikwa na umauti baada ya kuugua ghafla.

Taarifa hiyo imesema; Uongozi nwa Klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mchezaji wetu wa zamani Akilimali Yahya kilichotokea usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni baada ya kuugua ghafla.

“Simba inamuombea kwa Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi na awape subira ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiuki kigumu.”

error: Content is protected !!