October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba waja na ‘Iga Ufe’

Spread the love

KLABU ya Simba imezindua wiki yao rasmi kuelekea kilele cha tamasha lao la ‘Simba Day’ kitakachofanyika tarehe 6, Agosti 2019 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku wakiwa na kauli mbiu ya ‘Iga ufe’. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amesema tamasha hilo ni la mwaka wa 10 sasa toka 2009 na kuonesha mafanikio makubwa huku baadhi ya klabu zikiiga utamadui huo.

“Tumefanya hili tamasha huu ni mwaka wa 10 mfululizo, toka enzi za Mzee Dalali (Hassan) na Kaduguda (Mwina), na matarajio yetu hili jambo litakuwa endelevu kwa miaka yote ya uhai wa simba na jambo jema lazima liigwe,” alisema Manara.

Kuelekea kilele cha tamasha hilo Simba itarajia kufanya shughuli mbalimbali ndani ya wiki hii kama kuzindua jezi, kuwatembelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu, kuwatembelea wagonjwa hospitali sambamba na uchangiaji wa damu.

Siki hiyo pia Simba itarajia kutambulisha kikosi chao cha wachezaji na benchi la ufundi watakaotumika kwenye msimu wa ligi wa 2019/2020 sambamba na michuano ya klabu bingwa Afrika na kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Power Dynamos kutoka Zambia

error: Content is protected !!