Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba waachana na Pascal Wawa, kumuaga Alhamisi
Michezo

Simba waachana na Pascal Wawa, kumuaga Alhamisi

Spread the love

 

BENKI kisiki wa timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, Pascal Wawa ametangazwa kuachana na timu hiyo aliyoitumikia kwa misimu minne mfululizo kwa mafanikio makubwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wawa mwenye miaka 36, aliyezaliwa tarehe 1 Januari 1986, Bingerville nchini Ivory Coast alijiunga na Simba msimu wa 2017/18 akitokea Al-Merrikh ya Sudan ambako aliitumikia kwa msimu mmoja tu akitokea Azam FC ya Dar es Salaam.

Tangu alipojiunga na Simba, alikuwa beki tegemeo wa kati akicheza kwa mafanikio makubwa na kuwezesha kushinda makombe ya ligi kuu mara nne mfululizo, Kombe la Shirikisho mara tatu na kuisaidia kufika robo fainali Kombe la Klabu Bingwa Afrika.

Leo Jumanne, tarehe 21 Juni 2022, Simba imetumia kurasa zake za kijamii kutangaza kuachana na Wawa wakisema, “baada ya kutumikia timu yetu kwa misimu minne, Serges Pascal Wawa hatakuwa sehemu ya kikosi chetu cha msimu ujao.”

“Mkataba wake utamalizika mwisho wa mwezi huu na mchezo wa Alhamisi dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mchezo wake wa mwisho.”

Wawa anaondoka ndani ya timu hiyo akiiacha ikiwa imepotea makombe yote mawili iliyokuwa inayatetea ya ligi kuu pamoja na la shirikisho na ikishuhudia akiwa amepoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Ujio wa Joash Onyango raia wa Kenya na Enock Inonga maarufu Verane wa DR Congo ulimfanya Wawa kuwa chaguo la pili kwa makocha kadhaa walioifundisha timu hiyo.

Wawa alianza soka la kulipwa kwa ASEC Mimosas ya nchini mwake Ivory Coast kuanzia 2003-2010 kisha akatimukia Al-Merrikh ya Sudan alipocheza kuanzia msimu wa 2010 hadi 2014.

Alitimukia Azam kuanzia 2014 hadi 2016 aliporejea tena Al Merrikh alipocheza hadi 2017 na kujiunga na Simba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!