June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba Vs Yanga: Mashabiki kupewa barakoa bure

Spread the love

 

CHAMA cha soka Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania, kitagawa barakoa bure kwa mashabiki watakaoudhuria mchezo wa fainali kombe la shirikisho utakaowakutanisha Simba na Yanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Kigoma…(endelea).

Lengo ni kuwakinga mashabiki hao na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).

Mchezo huo utakaowakutanisha watani wa jadi, utafanyika kesho Jumapili tarehe 25 Julai 2021 huku ukitegemewa kushuhudiwa na watazamani 17,000 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.

Hayo yamesemwa na katibu wa chama cha soka mkoa wa Kigoma Omary Nindi, leo Jumamosi, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo wa watani wa jadi.

“Sisi kama chama cha soka mkoa wa Kigoma, katika mchezo wa kesho tumepanga kugawa barakoa bure kwa mashabiki wote watakaohudhuria mchezo huo, ili kujikinga na maambukizi ya wimbi la tatu la ugonjwa wa corona na kuchukua tahadhari kama serikali ilivyosema,” amesema Nindi

Barakoa hizo zitatoka kwenye bohari Kuu ya dawa (MSD) ambazo zitakuwa kwenye mageti yote nane yatakayotumiwa na mashabiki kuingia uwanjani hapo.

Aidha katibu huyo amesema licha ya kugawa barakoa hizo, lakini pia wataweka pia vitakasa mikono kwenye milango hiyo.

“Licha ya barakoa lakini pia kwenye mchezo huo wa kesho tutaweka maji pamoja na vitaka mikono (sanitizer) kwenye sehemu za milango ya kuingia uwanjani,” amesema

Kuelekea kwenye mchezo huo mpaka jana jioni jumla ya tiketi 12,000 zilishauzwa kati ya tiketi 17,000.

error: Content is protected !!