May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba uso kwa uso na Al Ahly, AS Vita na El Merreikh

Kikosi cha Simba

Spread the love

KLABU ya Soka ya Simba imepangwa kundi A, kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na klabu za Al Ahly kutoka nchini Misri, AS Vita kutoka DR Congo na Al Merreikh ya nchini Sudan. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Makundi hayo yamepangwa leo tarehe 8 Januari, 2021 kwenye droo iliyochezeshwa jijini Cairo, Misri ambapo Simba imepangwa tena na bingwa mtetezi wa michuano hii klabu ya Al Ahly pamoja na AS Vita ambao Simba alicheza nao mara ya mwisho aliposhiriki hatua hii ya raundi kwenye msimu wa 2018/19 na Simba alifanikiwa kufuzu hatua ya nane bora.

Kikosi cha Al Ahly

Kwenye kundi hilo Simba ataanza mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya AS Vita kutoka Congo ambapo mara ya mwisho kucheza dhidi ya timu hiyo Simba alifungwa mabao 5-0, na mara baada ya hapo Simba atarejea nyumbani Tanzania kuwakabili Al Ahly kutoka nchini Misri ambapo mara ya mwisho Simba alipata ushindi wa bao1-0.

Kikosi cha AS Vita

Mara ya mwisho Simba kushiriki hatua ya makundi ilikuwa msimu wa 2018/19 alikuwa kundi D, dhidi ya timu za Al Ahly, AS Vita na JS Soura na Simba ikafanikiwa kumaliza kwenye nafasi ya pili na kwenda hatua ya rob0 fainali na kupoteza mchezo huo mbele ya TP Mazembe.

Al Merreikh ya Sudan
error: Content is protected !!