November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba sasa kukutana na vigogo Afrika

Spread the love

BAADA ya Simba hapo jana kufanikiwa kuibuka ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Nkana FCkutoka Zambia, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa kukutana na vigogo wa soka Afrika katika hatua hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Simba katika hatua hiyo itakuwa pamoja na Al Ahly SC, TP Mazembe, Wydad AC, Mamelodi Sundown, AS Vita Club, Orland Pirates, CS Constantine, JS Saoura, Ismaily SC, Lobi Stars FC, FC Platnum, Horoya SC, CA Africain na Asec Mimosas.

Hatua hiyo ambayo makundi yake yanatarajiwa kupangwa Desemba 28, mwaka huu, imejaa utajili wa fedha na inaonekana kuwa ngumu kutokana na kujumuisha timu ambazo zinaonekana kuwa tishio na zinafanya vizuri kwenye soka la Afrika kwa miaka ya hivi karibuni.

Mpaka sasa Simba wameshafanikiwa kuvuta kitita cha shilingi bilioni 1 baada ya kufanikiwa kufuzu kwenye hatua hiyo ya makundi na huwenda wakapa fedha nyingi zaidi kama wakifanya vizuri na kufanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Michezo hiyo ya makundi amabayo inatarajiwa kuanza kuchezwa januari, 2019 baada ya CAF kubadiliosha utaratibu wa michuanio hiyo ili iwezealizika sawa na mashindano mengine katika nchi mbali mbali ili klabu ziptae muda wa kujiandaa na msimu mpya wa kimashindano tofauti na hapo awali.

error: Content is protected !!