
Wachezaji wa Bandari FC wakishangilia ushindi wao dhidi ya Simba na kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Sport Pesa
SIMBA imeondoshwa katika michuano Sport Pesa baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Bandari FC ya Kenya katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Meddy Kagere dakika ya 45, Bandari FC wakafanikiwa kusawazisha bao hilo kwa njia ya mkwaju wa penalti katika dakika ya 59 kupitia kwa William Wadri
Katika kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko na kuingiza wachezaji watano wakiwemo Emanuel Okwi, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Shiza Kichuya na Haruna Niyonzima lakini ilipofika dakika ya 72 mchezaji Wilberforce Lugogo alifanikiwa kuipatia Bandari FC bao la pili ambalo lilidumu mpaka mwisho na kufanikiwa kuingia fainali.
Ikumbukwe bingwa wa michuano hiyo atapata zawadi ya kombe na kiasi cha fedha Sh. 30 milioni sambamba na kucheza mechi na klabu ya Evarton FC inayoshiliki Ligi Kuu nchini England mwezi Julai mwaka huu.
Tazama mabao yote hapo chini
More Stories
Simba yamfukuzisha Kaze Yanga
Kocha mkongwe nchini ampigia chapuo Ndayilagije Yanga
Taifa Stars kuingia kambini leo, kuivutia kasi Guinea