May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba: mechi ya Yanga ni nyepesi

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba imeonekana kutouwazia mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya wapinzani wa karibu klabu ya Yanga, kwa kutanabaiasha kuwa malengo yao ya sasa niu kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Hayo yameibuliwa na Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally ambaye alizungumza na waandishi wahabari mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Orlando Pirates kwenye mchezo war obo fainali wa michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Ahamed alisema kuwa ndani ya mwezi huu wan nne, mchezo mgumu pekee uliosalia kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara ni mchezo wa marudiano utakaopigwa tarehe 24 Aprili 2022, dhidi ya Orlando nchini Afrika Kusini.

“Mechi liyobaki ngumu kwa mwezi wanne ni dhidi ya Orlando, ndio inaweza kutunyina usingizi kwa kushindwa kuingia hatua ya nusu fainali, Mechi pekee ambao tunaifikilia pamoja na kuwa na hamu nayo, kweli kweli mechi pekee zilizosalia ni kawaida.” Alisema meneja huyo

Ikumbukwe katika ndani ya mwezi huu wane, Simba itashuka dimbani Aprili 30 2022, kwenye mchezo dhidi ya Yanga kwenye Ligi Kuu bara kwenye duru la lala salama.

Aidha Ahmed alisema kuwa, wao kama Simba wameshahama kwenye mambo ya kuwekeza nguvu kwenye mchezo dhidi ya Yanga na kutanabaisha kuwa mikakati yao kwa sasa ni michuano ya kimataifa.

“Tumeshaahama kwenye kuwekeza nguvu kucheza na Yanga kwenye mchezo mmoja, tumshatoka kwenye dhana ya utani na kwa sasa mpira ni biashara.” Alisema Meneja huyo

Mpaka sasa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara klabu ya Yanga ipo kileleni wakiwa na pointi 51, tofauti ya alama 10 na Simba wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 41, huku wote wakiwa wamecheza michezo 19.

error: Content is protected !!