May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Mbeya City ni kufa au kupona

Spread the love

Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao utakaopigwa hii leo kati ya Simba dhidi ya Mbeya City, utakuwa na umuhimu kwa kila timu, kulingana na nafasi ya kila timu kwenye msimamo wa Ligi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo utapigwa hii leo, kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam majira ya saa 1 usiku ambapo Simba atakuwa mwenyeji.

Timu hizo zote mbili zinaingia kwenye mchezo huo, huku zikiwa na malengo tofauti kwa uhitaji wa pointi tatu kwenye mechi hiyo.

Kwa upande wa Simba wanaingia kwenye mchezo huo, huku wakiwa wanawaza taji la Ligi Kuu mara baada ya kubakisha alama saba, kabla ya kutangazwa kuwa mabingwa wapya kwa msimu 2020/21.

Pointi tatu za mchezo huo, zitawanufaisha Simba ambapo watakuwa wamesalia na pointi nne katika saba wanazozitafuta, kabla hawajakutana na matani zao Yanga kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu utakaopigwa tarhe 3 Julai, 2021.

Kabla ya mchezo wa leo, Simba ipo kileleni ikiwa na pointi 70, mara baada ya kucheza michezo 28, huku ikiitaji alama saba tu, kutangazwa kuwa mabingwa pointi ambazo hazitafikiwa na timu yoyote.

Kwa upande wa Mbeya City, anaingia kwenye mchezo huo huku akiwa kwenye nafasi ya hatari ya kushuka daraja kama hatopata matokeo.

Kabla ya mchezo huu wa leo, Mbeya City inashika nafasi ya 13, wakiwa na michezo 31 na pointi 36 na kama akifungwa kwenye mchezo huu wa leo anaweza kushuka mpaka nafasi ya 15, ambapo atakuwa kwenye nafasi ya kushuka daraja moja kwa moja na kusalia na michezo miwili.

Kuelekea mchezo huu hapo baadae, kocha msaidizi wa Mbeya City, Mathias Wandiba alisema kuwa, wao wamejiandaa na kupata matokeo ya ushindi licha ya kuwaheshimu Simba

“Ni mechi muhimu sana kwetu, lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata pointi tatu ambazo kwetu ni muhimu sana na hatuwezi kuwa daraja kwa simba.” Alisema kocha huyo

Aidha Wandiba alielezea hali za wachezaji wake, toka walipomaliza mchezo wao dhidi ya Costal Union kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Wachezaji wanahali nzuri na kila mtu yupo vizuri kucheza mechi ya kesho, sisi mipango yetu ni kushinda michezo minne ya mwisho, tulianza kushinda na Costal union na tunafuatia na Simba.”Aliongezea kocha huyo

error: Content is protected !!