August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba mambo magumu Mbeya

Spread the love

 

KLABU ya Simba imejikuta kwenye wakati mgumu, kufuatia kupoteza mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kukubali kichapo cha bao 1-0, dhidi ya Tanzania Prisons. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo wa mzunguko wa 29, ulipigwa kwenye dimba la CCM Sokoine jijini Mbeya ulishuhudia Simba kuwa kwenye wakati mgumu kwa matokeo hayo licha ya kutoathiliwa na chochote.

Bao pekee kwenye mchezo huo kutoka kwa Tanzania Prisons liliwekwa kambani na Benjamin Asukile kwenye dakika ya 53, na kufufua matumani ya timu hiyo kuepuka kushuka daraja.

Mchezo huo ulikuwa muhimu kwa Prisons ambaye mara baada ya kuibuka na alama hizo tatu, imefikisha jumla ya pointi 26 wakiwa kwenye nafasi ya 15, huku wakisalia mchezoa mmoja mkoni na endapo wakifanikiwa kushinda huwenda wakasogea mpaka nafasi ya 14.

Licha ya kupoteza mchezo huo, matokeo hayo bado hayawaathili chchote klabu ya Simba kwa kuwa wanaendelea kusalia kwenye nafasi yao ya pili wakiwa na pointi 60.

Kabla ya kupoteza mchezo huu wa hii leo, Simba ilifanikiwa kupata ushindi katika michezo mitatu mfululizo ya nyuma huku kikosi hiko, kikiwa chini ya kocha msaidizi Selemani Matola.

Ligi hiyo itafakia tamati Jumatano ya wiki hii tarehe 29, kwa kupigwa jumla ya michezo 15 katika viwanja tofauti, na kufanya msimu wa 2021/22 kufungwa rasmi.

error: Content is protected !!