Spread the love

 

 MARA baaada ya klabu ya soka ya Yanga hivi karibuni kutoa malalamiko yao kuhusu mwenendo wa waamuzi kwenye baadhi ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, uongozi wa klabu ya Simba umeibuka na kufunguka kuwa malalamiko yao hayana tija kwa sasa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Katika mkutano waliofanya na waandishi wa habari Jumanne ya tarehe 8 Februari 2022, moja ya malalamiko yaliyotolewa na klabu ya Yanga kupitia kwa Afisa habari wake Hassan Bumbuli na msemaji wao Haji Manara, yalilenga kuhusu wapinzani wao Simba kuongezewa dakika nyingi kwenye baadhi ya michezo yao.

Akijibu jambo hilo, akiwa kwenye moja ya kipindi cha radio, Meneja Mawasiliano na Habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally alisema kuwa, katika michezo yao miwili ya hivi karibuni walinda mlango wa timu pinzani walizokuwa wanacheza nazo walikuwa wanapoteza muda, mpaka kupelekea waamuzi kuwapa kadi.

“Tuangalie mechi mbili za mwisho, Mlinda mlango wa Tanzania Prison Benedict Haule, alioneshwa kadi kwa kupoteza muda, tuje mchezo wa Mbeya Kwanza mlinda mlango wao Hamad Kadedi naye alioneshwa kadi kwa kosa hilo hilo.”

“Huu muda ukafidiwe wapi? mpira uchezwe kwa dakika 70 au 80 haiwezekani, lazima muda uongezwe haya malalamiko yao hayanatija.” Alisema Meneja huyo

Hayo yote yanatokea wakati Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa mapumzikoni kwa wiki moja, ambapo itarejea tena kuanzia Ijumaa ya tarehe 21 Februari 2022, ambapo mpaka sasa Yanga ipo kileleni ikiwa na pointi 36, wakiwa na tofauti ya pointi tano na Simba waliokuwa kwenye nafasi ya pili wenye pointi 31.

Aidha Afisa Habari huyo aliendelea kufunguka kuwa, kwenye Ligi Kuu msimu huu wa 2021/22, idadi kubwa ya waamuzi waliofungiwa ni wale waliocheza michezo ya Yanga dhidi ya timu nyingine.

“Katika michezo ambayo mpaka sasa Simba tumecheza, hakuna mwamuzi aliyefungiwa kwa kushindwa kutafsili sharia, lakini katika michezo ya Yanga mpaka sasa wamefungiwa waamuzi wanne.

Ahmed aliwataja baadhi ya waamuzi hao, wakiwemo waliocheza michezo kati ya Yanga dhidi ya  Namungo na Polisi Tanzania.

“Mwamuzi Abel Willium aliyecheza mchezo wao dhidi ya Namungu alifungiwa, Hans Mabema aliyechezesha mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania nae alifungiwa.”

“Tafsiri yake ni nini? wapi wanapendelewa na wapi waamuzi wanawabeba?.” alisisitiza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *