Thursday , 30 March 2023
Home Kitengo Michezo Simba kushiriki michuano mipya Barani Afrika
Michezo

Simba kushiriki michuano mipya Barani Afrika

Spread the love

 

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itakutana Julai 16, 2021, nchini Morocco kujadili mfumo wa mashindano mapya ya (CAF Super League), ambayo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia (FIFA), Gianni Infantino ameyapa baraka. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Michuano hiyo inatarajia kushirikisha timu 20, ambapo kati ya hizo, timu 15 zimetajwa kushiriki ikiwemo Simba kutoka Tanzania.

Mashindano hayo, ambapo mapema mwaka huu yalishindikana kufanyika barani Ulaya (Europian Super League), sasa yamegeukia barani Afrika huku Rais wa sasa wa Shirikisho hilo, Patrice Motsepe akijinasibu kuwa yatakuza mpira wa Afrika.

Kwa mujibu wa mtandao wa Goal.com ulimnukuu Motsepe ambaye alinena kuwa dhumuni la michuano hiyo mipya limeshajadiliwa na wamejifunza kupitia barani Ulaya ambapo michuano hiyo ilishindikana.

“Tumeshafanya tathimini na mijadala ya awali itaanza na kuungwa mkono kwa mapana na wanufanika wa michuano hiyo.

Patrice Motsepe, Rais wa CAF

“Tumeangalia kwa namna gani, klabu kubwa barani Ulaya zilivyoshindwa kuunda michuano hiyo (European Super League) kutokana na uzoefu pamoja na changamoto zote walizopitia,” alifunguka Motsepe ambaye ameingia madarakani mwezi Machi, kuchukua nafasi ya Ahmad Ahmad.

Aidha Motsepe alisema kuwa anaamini wazo hilo, litasaidia kukuza mpira wa bara la Afrika ulimwenguni. “Itachangia mpira wa Afrika kuwa wa ushindani ulimwenguni,” alisema Rais huyo.

Michuano hiyo ambayo itakuwa na klabu 20 wanachama, na wengine wanaweza kushiriki kupitia michezo ya mtoano katika hatua ya awali.

Giann Infantino, Rais wa FIFA

Mtandao huo pia uliripoti kuwa Rais wa FIFA, Gian Infantino ambaye alipendekeza michuano hiyo kufanyika barani Afrika na kutabili kuwa baada ya miaka mitano wataingiza kiasi cha Sh. 6.9 trillioni.

Ukiacha Simba zingine timu ambazo mpaka sasa zitashiriki michuano hiyo ni Wydady na Raja Casablanca kutoka Morocco, Burkane, Al Ahly, Zamalek na Pyramids za Misri, Mamelod Sundowns, Orlando Pirates na Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini.

Wengine ni TP Mazembe na AS Vita za nchini DR Congo, Al Hilal, Al Merreikh kutoka Sudan na Horoya ya nchini Guinea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

error: Content is protected !!