May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba kusaka pointi 10 za ubingwa dhidi ya Polisi kesho

John Bocco mshambuliaji wa Simba

Spread the love

MARA baada ya mapumziko ya wiki mbili, hatimaye kikosi cha Simba kesho kitashuka Uwanjani dhidi ya Polisi Tanzania kutafuta pointi 10, Kwa ajili ya kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara kwa msimu 2020/21. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo utapigwa kesho jumamosi majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Ccm Kirumba, jiji Mwanza ambapo Polisi Tanzania watakuwa wenyeji.

Simba ambao tayari wapo Mwanza, wanaingia kwenye mchezo huo  huku wakihitaji ushindi katika michezo mitatu na sare moja.

Kwa sasa Simba wapo kileleni wakiwa na pointi 67, kama wakifanikiwa kupata alama 10 watakuwa na pointi 77, ambapo zitashindwa kufikiwa na klabu nyingine yoyote kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Yanga waliokuwa kwenye nafasi yapili kama wakishinda michezo yao mitano iliyobaki watafikisha jumla ya pointi 76, na uwezekana wa kuendelea kusalia kwenye nafasi ya pili.

Katika michezo iliyosalia ya Simba kutafuta alama hizo 10, wataanzania kesho dhidi ya Polisi Tanzania, na tarehe 22 juni watashuka tena dimbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuwaalika klabu ya Mbeya City.

Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Simba kitakuwa wenyeji kwa kuwakaribisha Yanga mchezo utakaopigwa tarehe 3 Julai 2021, huku mchezo ambao unaweza kuwapa fursa ya kutangaza ubingwa utakuwa dhidi ya Azam Fc utakaopigwa tarehe 14 julai 2021, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamaz

error: Content is protected !!