May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba kupaa Marekani

Spread the love

 

KLABU ya Simba inatarajia kuweka kambi ya maandalizi ya Ligi Kuu mwaka 2021/2022 nchini Marekani kwa ushirikiano wa klabu ya DC United inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini humo (MLS). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Mohamed Dewji ‘Mo Dewji’ amesema Simba itacheza mechi za kirafiki timu ya DC United pamoja na timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu nchini humo.

“Ni furaha kukutana na Jason Levie mmiliki wa timu ya DC United yenye thamani zaidi ya dola za Marekani milioni 700,” aliandika Mo katika akaunti yake ya Twitter.

Mo Dewji amesema hayo baada ya kukutana na moja ya wamiliki wa DC United Jason Levien (kwenye picha).

Kambi hiyo itakuwa ni ya awamu ya pili baada ya Morocco ambayo Simba inaendelea kujinoa.

error: Content is protected !!