March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba kumechafuka, mkutano wapingwa mahakamani

Hamis Kilomoni, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Simba (katikati) akitinga mahakamani Kisutu kupinga mkutano wa klabu hiyo

Spread the love

BODI ya Wadhamini wa klabu ya Simba imefungua kesi kupinga mkutano mkuu wa klabu hiyo, uliopangwa kufanyika Agosti 13, mwaka huu, anaandika Faki Sosi.

Bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo wamefungua kesi leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiiomba mahakama hiyo izuie kufanyika kwa mkutano huo.

Wakili wa bodi hiyo ya wadhamini, Juma Nassoro amesema kesi hiyo namba 188 ya mwaka 2017, ipo chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Wakili Nassoro amesema wateja wake wamefungua kesi hiyo kupinga wanaokaimu uongozi Klabu ya Simba kuitisha mkutano mkuu na kuendelea na maandalizi ya kubadilisha klabu hiyo kutoka mfumo wa kiuanachama na bodi ya udhamini na kuwa kampuni ya kibiashara.

Wamepinga suala hilo, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utaratibu huo haukubaliani na katiba ya Simba iliyosajiliwa na Rita mwaka 1975 na ndio imeunda bodi ya udhamini.

Hadi hivi sasa hakuna rekodi yeyote Rita inayoonyesha kwamba kuna katiba imebadilishwa na kuna mfumo mpya.

Hivyo wananchama wa Simba chini ya bodi ya udhamini imewapata muongozo wa kufungua kesi mahakama ni kupinga utaratibu unaofanywa na uongozi unaokaimu kufanya mabadiliko.

Moja ni suala la kikatiba na wanaokaimu hawana mamlaka, kwani kwa mujibu wa katiba utaratibu wa mikutano upo na waliopo hawajakidhi kwani inatakiwa Kaimu wa Rais wa Simba ndiyo aitishe.

Pia kitendo hicho ni kuhamisha umiliki wa Simba kwenda kinyime na Bodi ya Simba ambayo hadi sasa haijafutwa.

Hivyo leo ilikuwa ni kuzuia mkutano huo, hivyo mahakama inatarajia kesho kusikiliza pingamizi la upande wa wadaiwa.

Kabla ya kufikia uamuzi huo ambao utatolewa kesho bodi hiyo ya wadhamini uliuonya uongozi wa klabu hiyo kuachana na mipango ya maandalizi ya mkutano huo na kwamba kama wakiendelea basi itakwenda mahakamani kuuzuia.

Uamuzi huo wa bodi ya wadhamini ni kinyume na kanuni za Fifa inayokataza masuala ya mpira kwenda mahakamani hivyo kuna uwezekano wa Simba ikapoteza nafasi ya kushiriki Ligi Kuu pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

error: Content is protected !!