Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba kumalizana na ubingwa mapema
Michezo

Simba kumalizana na ubingwa mapema

Seleman Matola kocha msaidizi wa klabu ya Simba
Spread the love

KIKOSI cha klabu ya Simba leo kitashuka dimbani, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC, ambapo Kocha Msaidizi, Selaman Matola amesema wanataka kushinda mchezo huo ili kuwa mabingwa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo utapigwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, majira ya saa usiku.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Matola alisema kuwa, mara baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Yanga, sasa wanaingia kwenye mechi dhidi ya Kmc na kukili kuwa utakuwa mchezo mgumu.

“Mara baada ya kucheza mchezo wetu dhidi ya Yanga na kupoteza, najua sasa tunaingia kwenye mechi ya KMC najua nayo ni ngumu sio rahisi.

“KMC ni timu ngumu, inawachezaji wazoefu wanaojielewa ila tujiandaa kupata matokeo pamoja na ugumu huo ili tuweze kuwa mabingwa,” amesema Matola.

Simba mpaka sasa inapointi 73, ikiwa kileleni mara baada ya kucheza michezo 30, ambapo wanahitaji pointi nne, ilikufikisha alama 77 ambapo hazitafikiwa na timu yoyote kwenye msimamo wa Ligi.

Aidha Matola alinena kuwa, kupoteza mchezo wao dhidi ya Yanga hawakupenda, ila imetokea kwa kuwa nao walikuwa wakihitaji pointi hizo kuwa mabingwa.

“Tumefungwa sio kama tumependa ila tunahitaji kupata matokeo ili tuwe mabingwa kwenye mechi ya kesho,” aliongezea Matola.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!