BAADA ya kukubali kichapo cha bao 1-0, dhidi ya Al Ahly na kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi A, klabu ya Simba itacheza hatua ya robo fainali dhidi ya Cr Belouizdad, Horoya na MC Alger. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Simba atakutana na timu hizo ambazo zimeshika nafasi ya pili kwenye makundi yao na mchezo huo wa robo fainali wataanzia ugenini kwa sababu ni kinara wa kundi A.
Kwenye kundi A, Simba amemaliza akiwa na pointi 13 na nafasi ya pili ikishikwa na Al Ahly ikiwa na pointi 11.
Kwa mantiki hiyo kwenye mchezo wa robo fainali Simba atakuwa na faida ya kuanzia ugenini kati ya timu hizo tatu zilizoshika nafasi ya pili.
CR Belouizdad imeshika nafasi ya pili kwenye kundi B, nyuma ya Mamelodi Sundown wakiwa na pointi tisa, Holoya wao wameshika nafasi hiyo ya pili wakiwa kundi C, wakiwa na pointi 8, nyuma ya Wydad Casablanca.
MC Alger wameshika nafasi hiyo ya pili kwenye kundi D, wakiwa na pointi 8, nyuma ya ES Tunis iliyoongoza kundi hilo.
Michezo hiyo ya robo fainali itachezwa kuanzia tarehe 14 Mei 2021 na fainali ya michuano hiyo kwa msimu wa 2020/21 itachezwa tarehe 17 Julai, 2021.
Nakupata sana simba linZIMA WAENDE FAINALI