MARA baada ya kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa mara ya nne mfululizo, klabu ya Simba itakabidhiwa kombe hilo pamoja na medali, kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Namungo FC. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Mchezo huo, utapigwa tarehe 18 Julai 2021, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo ndiyo itakuwa tamati ya ligi hiyo.
Simba ilitangazwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo, tarehe 11 Julai, 2021, kufuatia kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union.
Mabingwa hao walifikisha jumla ya pointi 79, ambazo hazitafikiwa na timu yoyote kwenye msimamo wa ligi hiyo katika michezo miwili iliyosalia.
Leave a comment