August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba kujichimbia Morogoro

Kikosi cha Timu ya Simba

Spread the love

KATIKA kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara hatimaye kikosi cha Simba kitakwenda kuweka kambi kwa wiki mbili mkoani Morogoro chini ya makocha wao Joseph Omog na Jackson Mayanja kwa lengo kuendelea kufanya vizuri, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Taarifa hiyo ambayo ilitolewa kupitia ukurasa wa mtandao wa twitter wa klabu hiyo yenye lengo ya kuwafaamisha na kuwajulisha wapenzi na washabiki wa klabu ya Simba katika kujidhatiti na kuendelea na mbio zao za ubingwa kwa msimu huu.

Mzunguko huo ambao unatazamiwa kuanza Desemba 17 mwaka huu, huku kila timu ikijiimarisha kwa kufanya usajili mbali mbali za wachezaji kwa nia ya kuimalisha vikosi vyao kwa lengo la kupata matokeo chanya katika mzunguko huo wa pili.

Simba ambayo kwa sasa wanaongoza ligi wakiwa na pointi 35 katika mzunguko wa kwanza wa ligi, huku wakifuatiwa na mahasimu wao Yanga ambao wana alama 33 na kufanya kuwa na tofauti ya alama mbili mpaka sasa.

Katika hali nyingine klabu ya Simba imeshakamilisha usajiri wa mlinda mlango Daniel Agyei ambaye alikuwa akichezea klabu ya Medeama inayo shiriki ligi kuu nchini Ghana kwa mkataba wa miaka miwili huku akitazamiwa kuleta upinzani mkali kwa mlinda mlango wa sasa Vicent Angban.

error: Content is protected !!