Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Michezo Klabu Bingwa Afrika, Simba kuivaa Plateau United ya Nigeria
Michezo

Klabu Bingwa Afrika, Simba kuivaa Plateau United ya Nigeria

Spread the love

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba itaivaa klabu ya Plateau United kutoka nchini Nigeria kwenye michezo ya awali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika inayotarajiwa kuchezwa Decemba mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dat es Salaam … (endelea).

Droo hiyo ambayo ilipangwa leo na Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) huku ikionesha kuwa Simba ataanzia ugeneni nchini Nigeria katika kusaka nafasi ya kufuzu kwa hatua ya mzunguko wa kwanza.

Plateau United wamefanikiwa kuingia hatua mara baada ya kuwa mabingwa wa Ligi Kuu nchini Nigeria kwa kucheza michezo 25 na kukusanya pointi 49 licha ya Ligi hiyo kutomalizika kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19.

Mara ya mwisho timu hiyo kushiriki michuano ya klabu bingwa ilikuwa 2018 ambapo ilitolewa kwenye mzunguko wa kwanza na klabu ya Etoile du Sahel ya nchini Tunisia kwa mabao 4-2 katika michezo yote miwili.

Kama Simba itafanikiwa kuwaondosha Plateau United kwenye hatua hiyo basi itakutana kati CD do Sol ya Msumbiji au FC Platnum ya nchini Zimbabwe kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Mchezo huo wa awali katika mzunguko wa kwanza kati ya Plateau dhidi ya Simba unatarajiwa kuchezwa kati ya 27-29 Novemba 2020, na marudio yanatarajiwa kufanyika kati 4-6 Decemba 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!