May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba kuifuata Al Ahly jioni ya leo

Spread the love

 

KIKOSI cha wachezaji pamoja na viongozi wa klabu ya Simba wataondoka jioni ya leo tarehe 6 Aprili, 2021, kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa kundi A, utachezwa tarehe 9 Aprili, 2021 huku Simba ikiwa tayari imeshakata tiketi ya robo fainali ya michuano hiyo.

Kikosi hiki kitaondoka Jijini Dar es Salaam 9:25 na Shirika la ndege la Emirates mpaka Dubai na kisha kesho Jumatano asubuhi wataanza safari ya kwenda Cairo ambapo watafika majira ya 4:05 asubuhi.

Simba inaenda kucheza mchezo huo huku wakiwa vinara kwenye kundi A, wakiwa na pointi 13 mara baada ya kushinda michezo minne na kwenda sare mmoja.

Mpaka sasa Simba kwenye kundi hilo hajapoteza mchezo wowote na akiwa ameruhusu bao moja tu.

Katika michezo ya ugenini Simba aliyocheza kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu hajapoteza.

Simba amefanikiwa kuifunga AS Vita nchini Congo na kutoka sare ya bila kufungana na Al Merrreikh kwenye mchezo wao uliochezwa Sudan.

error: Content is protected !!