May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba hali mbaya, wakubali kipigo mbele ya Kagera

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba imejikuta kwenye wakati mgumu kufuatia kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar kwa bao 1-0. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo wa Ligi Kuu ambao ulikuwa wa kiporo, ulipigwa hii leo kwenye dimba la Kaitaba, mkoani Kagera majira ya Saa 1o jioni.

Lilikuwa bao la dakika ya 71, kutoka kwa mshambuliaji mkongwe, Hamis Kiiza ambaye alikuwa anacheza mchezo wake wa pili, toka aliposajiliwa na Kagera Sugar kwenye dirisha dogo la ysajili akitokea Uganda.

Kufuatia kupoteza mchezo huo, Simba inaacha jumla ya point inane katika michezo mitatu mfululizo waliocheza, toka waliporejea kwenye kombe la Mapinduzi.

Katika michezo hiyo mitatu Simba walianza kupoteza kwa bao 1-0, dhidi ya Mbeya City, kisha walikwenda sare ya bila kufungana.

Katika michezo hiyo mitatu, inawafanya Simba kucheza jumla ya dakika 270, bila kupata bao lolote, huku upande wao ukiruhusu mabao mawili.

Kwa matokeo hayo, yanawafanya Simba kusalia kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 25, mara baada ya kucheza michezo 13, pointi 10 nyuma ya Yanga ambao nivinara wa Ligi hiyo wakiwa na alama 35.

error: Content is protected !!