Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Simba dhidi ya AS Vita, mashabiki ruksa
Michezo

Simba dhidi ya AS Vita, mashabiki ruksa

Barbara Gonzalez, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba
Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeiruhusu klabu ya Simba kuingiza mashabiki kwenye mchezo wao dhidi ya AS Vita kutoka Jamhuri ya Congo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa kundi A, utapigwa Jumamosi tarehe 3 Aprili 2021, kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 10 jioni.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari hii leo, Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa leo wanafuraha mara baada ya kuruhusiwa kuingiza mshabiki kwenye mchezo huo.

“Leo tumepata habari njema kutoka CAF kuwa tumeruhusiwa mashabiki 10,000 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club.

“Hii ni fursa ya kipekee ambayo tumeipata, hakuna timu imeruhusiwa kwa idadi hii, masharti ni mengi na lazima tuzingaitie taratibu walizoweka,” alisema Barbara.

Haji Manara, Afisa Habari wa Simba

Ruksa hiyo imekuja kufuatia katazo lililowekwa mara ya kwanza ya klabu hiyo kutocheza bila mashabiki kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Merreikh ya Sudan uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa Afisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara amesema kuwa hali ya kikosi kipo vizuri na hakuna majeruhi yoyote na wachezaji waliokuwa kwenye timu zao za Taifa wameshaanza kuwasili kambini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!