October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba Day: TP Mazembe kuwasilia leo

Spread the love

 

KIKOSI cha wachezaji 23 wa timu ya TP Mazembe ya Congo kinawasili nchini Tanzania leo Jumamosi, tarehe 18 Septemba 2021. Anaripoti Hunda Mintanga, TUDARCo … (endelea).

TP Mazembe wanakuja kunogesha kilele cha tamasha la Simba Day linalohitimishwa kesho Jumapili, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Katika tamasha hilo, Simba ambaoni mabingwa mara nne mfululizo wa ligi kuu Tanzania Bara, watatambulisha wachezaji wake itakaowatumika katika msimu ujao.

Pia, kutakuwa na buradani mbalimbali kutoka kwa wasanii na michezo ya awali ya mipira wa miguu kwa timu zake za vijana na wanawake.

TP Mazembe ambao wamewahi kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika, wataumana na Simba ambayo iliweka kambi jijini Arusha na jana Ijumaa usiku,imerejea Dar es Salaam.

error: Content is protected !!