May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba bado pointi mbili kuishusha Yanga

Spread the love

 

USHINDI wa mabao 2-0, ulitosha kuifanya Simba kuondoka na pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo ulipigwa hii kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera na kufanya Simba kufikisha pointi 55 wakiwa wamecheza michezo 23, nafasi ya pili nyuma ya Yanga wenye pointi 57, wakiwa na michezo 26.

Bao la Kwanza la Simba kwenye mchezo huo lilifungwa na Luis Miquisone kwenye dakika ya 12 ya mchezo mara baada ya kupokea pasi kutoka kwa Clotous Chama na kuandika bao lake la sita kwenye Ligi Kuu Bara.

Simba iliendelea kutawala mchezo na kufanikiwa kuandika bao la pili kupitia kwa Chriss Mugalu na kukamilisha idadi ya mabao mawili yaliyodumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu lakini Simba hawakufanikiwa kuongeza bao lolote na kufanya mpira huo kukamilika kwa mabao 2-0.

Baada ya mchezo huo Simba itasafiri kuelekea Misungwi mkoani Mwanza kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Gwambina FC, ambao jana walikubali kichapo cha mabao 3-1, dhidi ya Yanga.

error: Content is protected !!