December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Azam FC zabanwa ugenini, Yanga, Mtibwa Taifa kesho

Kocha wa Simba, Goran Kapunovic akitoa maelezo kwa wachezaji wake

Spread the love

MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu Tanzania bara umeanza leo huku matokeo ya sare yakitawala katika michezo sita iliyochezwa leo kwenye viwanja tofauti tofauti. Anaripoti Erasto Stansalus ….. (endelea).

Simba ambao walikuwa ugenini kwenye uwanja wa Mkwakwani walijikuta wakiambulia pointi moja baada ya kutoka suluhu na Coastal Union katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa katika dakika zote za mchezo huo. Kwa matokeo hayo Simba imefikisha point 17 na kuendelea kubaki katika nafasi yake ya 9.

Katika mechi nyingine Azam imelazimishwa sare ya mabao 2-2 na Polisi Morogoro katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, mabao ya Azam yakifungwa na ndugu, Kipre na Bolou Tchetche.  Kwa matokeo hayo Azam FC imerudi kileleni kwa kufikisha point 22 sawa na Yanga tofauti ikiwa ni idadi ya magoli.

[pullquote]MATOKEO MECHI ZA LEO 
Coastal  0-0 Simba 
JKT Ruvu  1-1 Mbeya City
Ndanda FC 1-1 Stand United
Polisi Moro 2-2 Azam FC
Prisons 1-1 Ruvu Shooting
Kagera 1-0 JKT Mgambo[/pullquote]

Katika mchezo mwingine Kagera Sugar baada ya kubadili uwanja wa nyumbani kutoka CCM Kirumba Mwanza na kuhamia Kambarage Shinyanga, leo imefanikiwa kuichapa Mgambo JKT bao 1-0 na kufikisha point 18.

Stand United ambao walikuwa wageni wa Ndanda FC katika uwanjani Nang’wanda Sijaona, mjini Mtwara, nao wameilazimisha sare wenyeji wao ya bao 1-1.

Mbeya City walikuwa wakikabili JKT Ruvu mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Chamanzi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, na mchezo huo umemalizika kwa sare ya bao 1-1.

Maafande wa Prisons wakiwa kwenye Uwanja wa nyumbani wa Sokoine jijini Mbeya, wameshindwa kuutumia vizuri uwanjani huo baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Ruvu Shooting.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mchezo mmoja kati ya Yanga na Mtibwa Sugar utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

error: Content is protected !!