MSEMAJI wa Kambi Rasimi ya Upinzani Bungeni, wa masuala ya fedha na uchumi David Silinde, ameitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya askari wa usalama barabarani ambao hufanya kazi bila weledi na kuwabambikizia makosa watu kwa lengo la kuomba rushwa, anaandika Dany Tibason.
Silinde ameyasema hayo wakati akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2017/2018, ambapo amedai kuwa ana taarifa kuwepo kwa utaratibu usio rasmi wa kuwapangia maofisa usalama barabarani kukamata magari na kukusanya kiwango maalum cha faini.
“Askari wa usalama barabarani wamekuwa wakisema kuwa wanalazimishwa kupeleka kiasi cha fedha kitokanacho na makusanyo ya faini za makosa ya barabarani, wasipofanya hivyo askari hao hunyimwa mafunzo au kuondolewa katika kitengo cha usalama barabarani,” amesema.
Katika hatua nyingine hatua nyingine, Silinde amekosoa uamuzi wa serikali wa kurasimisha wafanyabaiashara ndogo ndogo (machinga). wakiwemo Mama lishe na washehereshaji (MC) ambapo alidai uamuzi huo unalenga kuwabebesha mzigo wa kodi wajasiriamali hao wenye mitaji midogo.
Leave a comment