NAIBU Waziri Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), David Silinde ameagiza halmashauri zote nchini Tanzania, kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini kwa kukosa madawati au kusoma chini ya miti. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).
Silinde amesema, maeneo yenye upungufu wa madarasa kunapaswa kujengwa katika wilaya zote ambao uanze mara moja kwa yale maeneo yenye upungufu wa madarasa.
Hayo ameyasema leo Jumamosi tarehe 23 Januari 2021 alipotembelea shule ya msingi King’ongo iliyopo wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam kufatia agizo la Rais John Magufuli la kutaka ujenzi wa madarasa ya shule hiyo ukamilike haraka.
Silinde amesema, Serikali ilitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa maeneo mengi ya nchi katika mradi wa lipa kwa matokeo EP4R tangu Juni 2020.
https://youtu.be/gEMNicztSyk
Hata hivyo, Silinde amesema, madarasa bado hayajakamilika katika baadhi ya maeneo lakini ujenzi wa madarasa katika shule ya King’ongo yanakamilika kwa wiki zisizo zidi tatu na kutaka watendaji katika wilaya zote kukamilisha ujenzi bila kusukumwa na viongozi wa kubwa wa nchi.
“Tunaweza kutekeleza miradi mingi kwa wakati bila kusubili kushukumwa nah ii inaashilia sisi viongozi hatuwajibiki ipasavyo,” amesema Silinde ambaye pia Mbunge wa Tunduma (CCM).

Amesema, agizo la Rais Magufuli si kwa Ubungo au shule ya Kiny’ongo pekee bali ni la halmashauri zote nchini “na sisi hatutakubali hili. Halmashauri zote, kama kuna watoto wanakaa chini, tufanye kwa muda mfupi ili watoto warudi darasani.”
Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic amemweleza Silinde ujenzi wa madarasa huo utakamilika tarehe 31 Januari 2021 na mpaka tarehe 5 Februari, 2021 wanafunzi wataanza kuyatumia madarasa hayo na mpaka kukamilika yatatumia zaidi ya Sh.205 milion.
Amesema ujenzi wa vyumba tisa ambavyo vitakua na madawati yake pamoja ujenzi wa choo chenye matundu 12.
Tarehe 18 Januari 2021, Rais Magufuli akizindua majengo ya Shule ya Wavulana Ihungo iliyoko Bukoba Mkoa wa Kagera, alitoa maagizo kwa viongozi wa jijini la Dar es Salaam, kuhakikisha wanatatua changamoto ya shule hiyo.

Rais Magufuli aliwataka viongozi wenzake ndani ya Serikali “mahali ambapo kuna mapungufu mbalimbali tuyashughulikie” ili
kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
“Lakini kuna maeneo hata Dar es Salaam, kuna mapungufu, kuna shule moja ya msingi Ubungo Dar es Salaam (King’ongo), ina wanafunzi wengi tu, shule hiyo iko Dar es Salaam, Ubungo bado wanakaa chini.”
“Madarasa mengine yamebomoka, madawati yamevunjika na yameachwa, mkuu wa wilaya yupo, mkuu wa mkoa yupo, mkurugenzi yupo bado anakusanya kodi,” alisema Rais Magufuli na kuwataka kumaliza tatizo hilo ili pindi atakaporejea Dar es Salaam na kwenda kuitembelea, akute imemalizika na wananchi wanasomea darasani badala ya nje
Leave a comment