January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Silinde ainanga serikali bungeni

Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde

Spread the love

MBUNGE wa Mbozi Magharibi, David Silinde, (Chadema), ameishambulia serikali kwa kukwamisha miradi ya maji katika Wilaya ya Momba, Mbozi Magharibi kutokana na kushindwa kupata fedha za wahisani kutoka Ubeligiji. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

“Serikali ya imekuwa ikifanya uzembe katika kufuatilia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kushindwa kufuatilia fedha ya miradi ya maji katika Wilaya ya Momba na Mbozi magharibi ambazo zilitakiwa kutolewa na serikali ya Ubeligiji,” amesema Silinde.

Silinde alitao tuhuma hizo wakati wa kipindi cha maswali na majibu na kuitaka serikali ieleze ni kwanini imeshindwa kufuatilia fedha hizo ambazo zilitakiwa kutolewa.

Awali katika swali la msingi mbunge huyo alitaka serikali ieleze ni lini itatekeleza ahadi za rais alizozitoa mwaka 2010 za kuwapatia maji ya uhakika wananchi wa tunduma.

“Wakati wa kampeini za uchaguzi wa mwaka 2010 Rais Kikwete aliahidi kuwapatia maji salama nay a uhakika wananchi wa Tunduma,lakini mpaka sasa muda wa rais kutawala unamalizika na ahadi hiyo bado haijatekelezwa.

“Je ni lini serikalai ahadi hiyo itatekelezwa kama rais alivyoahidi” amehoji.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Maji, Amoss Makala,amesema  ni kweli wahisani hao wana malengo ya kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya maji.

Amesema  serikali ya ubeligiji  itatoa kiasi cha euro milioni 150  kwa ajili ya miradi ya maji katika Wilaya ya Momba, Mbozi Magharibi pamoja na Wilaya Tunduma.

Akizungumzia kuhusu ahadi za rais alisema ahadi zote za rais zinatekelezeka.

Amesema  mpaka sasa serikali imetumia sh.milioni 404.8 kuanzia mwaka wa fedha 2009/10  hadi 2014/15  na katika mwaka wa fedha 2016 serikali imetenga sh.milioni 300 ili kuendelea kuboresha huduma za maji.

error: Content is protected !!