April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Silinde kuikimbia Chadema?

David Silinde, aliyekuwa Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Uchumi

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ni wadhamini tu, wakishindwa kunidhamini kwenye uchaguzi, nitarudi kwa wapiga kura kupitia wadhamini (chama) wengine. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ni kauli ya Davidi Silinde, Mbunge wa Momba, Songwe aliyoitoa alipohojiwa na gazeti la Mwananchi kuhusu hatma yake ndani ya chama hicho, baada ya kukaidi amri ya chama Chadema ya kutohudhuria vikao vya bunge.

“Walionituma bungeni ni wananchi wa Momba na Chadema ni mdhamini tu, hivyo chama kinaweza kumdamini na wananchi wakikataa nisingekuwa mbunge.

“Kama Chadema wakikataa kunidhamini, naweza kudhaminiwa na chama kinginena na wananchi wakiamua, watanirudisha hapa. Hivi vyama ni udhamini tu lakini waamuzi ni wananchi,” amesema Silinde.

Silinde alitangaza kujizulu nafasi ya katibu wa wabunge wa chama hicho kuanzia tarehe 4 Mei 2020, kwa maelezo alishindwa kusimamia maagizo ya chama ya kutohudhuria bungeni.

Mwishoni mwa wiki, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, aliwataka wabunge wote wa chama chake kutohudhuria vikao vya Bunge.

Mbowe alisema, sababu ni kujiweka karantini kwa siku 14 ili kuangalia afya zao kama wana maambukizi ya virusi vya corona au la.

Hata hivyo, wabunge 11 Silinde, walikaidi uamuzi huo wa chama hicho kikuu cha upinzani na kuamua kuhudhuria mkutano wa Bunge ambao ulikuwa ukijadili mapato na makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Wabunge wengine walioingia bungeni ni; Joseph Selasini (Rombo), Anthony Komu (Moshi Vijijini), Peter Lijualikali (Kilombero), Jafary Michael (Moshi Mjini) na wabunge viti maalumu, Ratifa Chande, Mariam Msabaha na Sabrina Sungura.

error: Content is protected !!